News

Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini wasitisha mgomo

Published

on

Viongozi wa Muungano wa Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini UASU na wale wa Wafanyikazi wa vyuo vikuu KUSU wamekubaliana kusitisha mgomo wao uliyodumu kwa takriban siku 49.

Viongozi hao wakiongozwa na Katibu mkuu wa Muungano wa UASU Constantine Wasonga walisema wamesitisha mgomo huo baada ya kuafikiana masuala kadhaa ambayo serikali ilikuwa bado haijaweka wazi.

Viongozi hao waliwaagiza wahadhiri wote wa vyuo vikuu na wale wa wafanyikazi kurejea kazini mara moja kuanzia siku ya Jumatatu ili kuendelea na masomo.

Katika kikao na Wanahabari baada ya mazungumzo na viongozi wa serikali yaliodumu kwa masaa kadhaa, Wasonga alisema wamekubali pendekezo la serikali la kuwalipa malimbikizi ya fedha zao kwa awamu mbili.

Aidha walisema wameafikiana kwamba kati ya shilingi bilioni 7.9 ambazo walikuwa wakidai serikali kulingana na mkataba wa makubaliano wa CBA, shilingi bilioni 3.8 zitalipwa mwezi Novemba na shilingi bilioni 3.8 zengine zikilipwa mwezi Juni mwaka 2026.

Kwa upande wake Waziri wa elimu nchini Julius Migos Ogamba alisema serikali itatimiza ahadi iliyoweka kwa wahadhari hao, akisema mkataba uliyotiwa saini kati ya serikali na viongozi wa vyama vya wahadhiri utatekelezwa kikamilifu.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version