News

Wahudumu wa pikipiki za umeme Kilifi walalamikia mabadiliko ya bei za kubadili batri

Published

on

Wahudumu wa pikipiki za umeme mjini Kilifi kaunti ya Kilifi wameandamana wakilalamikia mkanganyiko ulioibuka upande wa bei za kubadili batri pamoja na huduma za pikipiki hizo.

Wakizungumza mjini Kilifi wahudumu hao walisema mabadiliko ya bei za batri za pikipiki hizo yamewachangia kupata hasara kutokana na mda wa matumizi kulingana na urefu wa mwendo, vile vile bei za kuzibadilisha kituoni.

Wakiongozwa na Benson Safari Thuva, wahudumu hao walisema batri za sasa hazidumu wa matumizi yao wakishinikiza kampuni inayosimamia pikipiki hizo kuangazia matatizo hayo.

Wahudumu hao walisema wanapitia ugumu wa kutengeneza pikipiki zao wakati zinapoharibika kutokana na uhaba wa vituo vya kurekebisha pikipiki, vile vile wamekuwa wakizuiwa na wahudumu wa vituo vya kuuza mafuta wakati wanapohitaji huduma za kujaza upepo.

Waliitaka serikali kupitia kwa rais William Ruto kuilingilia kati masaibu wanayopitia wanaboda boda nchini, wakisema wanaingia hasara ilihali wanamajukumu mengi ya kifamilia.

Kwa upande wake afisa msimami wa mradi katika kampuni ya pikipiki hizo za Spyro Baraka Underson alisema mabadiliko hayo yalitokana na malalamishi ya wahudumu wenyewe japo kwa sasa yanaangaziwa.

Taarifa ya Joseph Jira

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version