News
Wakaazi wa Bamba walalamikia ukosefu wa maji safi
Wakaazi wanaoishi katika vijiji vya Mitsemereni, Goshi na Kavunzoni katika wadi ya Bamba eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi wanalia ngoa kutokana na changamoto za kimaisha.
Wakaazi hao walisema tatizo la maji limekuwa donda sugu na kwamba wamekuwa wakitegemea maji ya vidimbwi vinavyojulikana kama Mitsara, kwa kunywa, matumizi ya nyumbani, kunyishwa mifugo na sasa wanagawana rasilimali hiyo na wanyamapori hasa Ndovu ambao wanatishia usalama wao.
Wakaazi hao walisema wanapitia changamoto nyingi katika kutafuta bidhaa hiyo muhimu licha ya viongozi wa eneo hilo kuahidi kulitatua suala hilo lililodumu kwa miaka mingi bila ya suluhisho.
Kulingana na simulizi za wakaazi hao, wengi wanaishi kwa hofu kutokana na wanyamapori kutangamana na binadamu hasa Ndovu waliitaka shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS kuingilia kati suala hilo na kuwanusuru katika hali hiyo ngumu ya maishja.
Taarifa ya Lolani Kalu