Business

Wakulima Kilifi Wakadiria Hasara, Wakosa Mahali pa Kupeleka Mazao

Published

on

Wito umetolewa kwa serikali ya kaunti ya Kilifi kujenga ukumbi maalum ambapo wakulima wataweza kupeleka mazao yao.

Kulingana na mwenyekti wa soko la magarini kaunti ya kilifi Mtawali Kenga wakulima wengi wamekosa soko la kupeleka bidhaa zao hali ambayo inapelekea kukadiria hasara kubwa.

Akizungumza na cocofm kenga amebainisha kuwa kwa sasa wakulima wanapeleka bidhaa zao sokoni pamoja na wafanyibishara mbalimbali hali ambayo inapunguza idadi ya wateja na kuwasababishia hasara kubwa.

Aidha Kenga ameitaka serikali kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wakulima wanatengewa soko maalum kando na wachuuzi ili kupunguza msongamano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version