Business

Wakulima Tanariver waeleza matumaini ya mazao bora

Published

on

Wakulima katika mradi wa unyunyizaji maji mashamba katika mradi wa Hola irrigation Scheme Kaunti ya Tanariver wameeleza matumaini ya kupata mazoa bora kufuatia hatua ya serikali kubadili mfumo wa mitambo ya usambazaji maji.

Walisema mitambo ya jereneta iliyokuwa ikitumia mafuta ilikuwa na gharama ila kwa sasa hatua ya serikali kuekeza katika mpango wa umeme utachangia faida zaidi.

Kulingana na Maurice Adero na Ernest Akumu changamoto ya maji vile vile utumizi wa mafuta kuendesha mitambo ya usambazaji maji vilichangia wakulima kupata hasara.

“Hapo nyuma kilimo chetu kilikuwa na shida kidogo mambo ya maji kwa sababu ilikuwa unapopanda mimea huwezi vuna kabla hujapata tatizo la kukosa maji, sasa tumetoka kwa donda sugu la mambo ya dizeli, kitambo dizeli inunuliwe mpaka ifike Tanariver pengine ipelekwe kwa vituo vya kusambaza maji ilikuwa na changamoto nyingi”, walisema wakulima hao.

Katibu wa idara ya unyunyizaji maji nchini Ephantus Kimotho alisema hatua hii itapunguza gharama za uendeshaji miradi kwa asilimia 70.

“Kwa mwezi ilikuwa ikitumia dizeli ya zaidi ya shilingi milioni 10, mamlaka ya unyunyizaji nchini imeweza kuunganisha na umeme na sasa mradi huu utakuwa ukiokoa asilimia sabini ya pesa hizo”, aliweka wazi Kimotho.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version