Business
Wakulima wa korosho walalamikia mazao duni
Wakulima wa korosho eneo la pwani wanalalamikia mazao duni kutokana na uvamizi wa wadudu kwenye mimea yao.
Kulingana na wakulima hao, mmea huo ulivamiwa na wadudu hali inayowasababishia hasara kwani mazao ni duni ikilinganishwa na pesa wanazotumia kuendeleza Kilimo hicho.
Wakizungumza na vyombo vya habari wakulima hao waliitaka serikali kuu na zile za kaunti kuhakikisha kwamba kuna dawa za kuangamiza wadudu hao ili kuwasaidia kuimarisha mazao yao.
Wakati huo huo waliitaka serikali kuandaa warsha ili kuwaelimisha wakulima kuhusu mbinu za kisasa za kilimo na kuongeza mazao yao wakisema kuwa wengi wa wakulima eneo la Pwani bado wanatumia mbinu za kitambo.
Taarifa ya Pauline Mwango