News

Wamiliki wa ardhi Mombasa wapewa makataa

Published

on

Serikali ya kaunti ya Mombasa imetangaza kipindi cha siku 45, kuanzia tarehe 1 Aprili, kwa wamiliki wa ardhi kulipia ada zao za umiliki wa ardhi (land rates) katika kaunti hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi yake, gavana Abdulswamad Shariff Nassir alisema hatua hiyo imefikiwa kufuatia mashauriano kati yake na Waziri wa fedha.

Nassir alisema kuwa serikali ya kaunti inadai zaidi ya shilingi bilioni moja, fedha ambazo zingesaidia kuimarisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa wale ambao bado hawajakamilisha malipo yao wanapaswa kutumia fursa hiyo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kabla ya muda wa siku 45 kukamilika.

Aidha, gavana huyo alionya kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wamiliki wa ardhi watakaoshindwa kulipa ada hizo baada ya kipindi hicho kumalizika.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version