News
Wanaharakati mjini Mombasa wamtaka Eliud Lagat kujiuzulu
Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu kaunti ya Mombasa wamefanya maandamano ya amani katikati mwa jiji la Mombasa wakimtaka Naibu Inspekta jenerali wa Polisi Eliud Lagat kujiuzulu.
Wanaharakati hao walisema hafai kujiondoa afisini kwa muda bali kujiuzulu ili kuruhusu uchunguzi kuendelea.
Wanaharakati hao ambao walibeba mabango ya kutaka haki itendeke kufuatia mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang’ aliyefarika katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi, walimtaka Lagat kuzingatia shinikizo la wananchi na kujiuzulu.
Hali sawia na hiyo ilishuhudiwa katika kaunti ya Kilifi ambapo vijana wa chuo kikuu cha Pwani pamoja na baadhi ya wanaharakati waliongoza maandamano ya Amani kauli mbiu ikiwa ni Eliud Lagat kujiuzulu huku wakimnyooshea kidole cha lawama Rais William Ruto.
Aidha alidai kwamba serikali ameshindwa kudhibiti visa vya polisi kutumia nguvu kupita kiasi na mauwaji ya kiholela nchini.
Haya yanajiri huku vijana wa kizazi cha Gen-Z wakifanya mandamano katikati mwa jiji la Nairobi wakishinikiza haki kutendeka na serikali kuwajibikia mauwaji hayo na kuwataka wote waliohusika kukabiliwa kisheria.
Taarifa ya Elizabeth Mwende