News

Wanaharakati wa Kenya Bob Njangi na Nicholas Oyoo waachiliwa huru

Published

on

Hatimaye wanaharakati Bob Njagi na Nicholas Oyoo wameachiliwa huru, siku 38 baada ya kutekwa nyara nchini Uganda wakisema walizuiliwa na jeshi la nchi hiyo kwa muda huo wote.

Wakizungumza muda mfupi baada ya kuwasili jijini Nairobi, Njagi na Oyoo walisema waliteswa mikononi mwa kikosi maalum cha jeshi la Uganda.

Wawili hao waliwashukuru wakenya kwa juhudi zao za kushinikiza waachiliwe.

Awali serikali ya Uganda ilikana kwamba wanaharakati hao walikuwa wanazuiliwa nchini humo.

Hata hivyo watetezi wa haki za binadam walieleza wasiwasi wao kuhusu taswira hii ya ukiukaji wa haki za kimsingi.

Njagi na Oyo waliachiliwa huru na kusafirishwa hadi mpaka wa Kenya eneo la Busia wakiandamana na Balozi wa Kenya nchini Uganda.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version