News

Wanaharakati wapinga ndoa ya jinsia moja Mombasa

Published

on

Vuguvugu la kupinga mahusiano ya jinsia moja mjini Mombasa limelalamikia bondi wanazopewa washukiwa wa kesi za ulawiti, wakisema pesa hizo huwa ni chache mno hali ambayo husababisha wanaotekeleza vitendo vya ulawiti huzidisha uovu huo.
Mwenyekiti wa vuguvugu hilo Salim Karama alisema hali hiyo imewafanya washukiwa wa ulawiti kuachiliwa kirahisi, wakitaka marekebisho kufanywa kwa vipengee vya kisheria ili kupunguza na hata kukomesha visa hivyo.
Karama aliitaka Idara ya Mahakama kuzichukulia kesi hizo kwa uzito ili kulinda kizazi kichanga kwani visa hivyo vinapoongezeka ni chanzo cha kupoteza kwa jamii na vijana wadogo ambao wanafaa kuwa mstari wa mbele kuchangia malengo elndelevu ya taifa sawa na kuheshimu mafunzo ya mwenyezi Mungu.
“Tunaitaka idara ya Mahakama nchini kuwa mstari wa mbele kukemea uovu huo pamoja na kuhakikisha haki kwa wale wanaotendewa unyama huo na kama Vuguvugu la kupinga mahusiano ya jinsia moja tutaendelea na shinikizo zetu kupinga uhalifu huu kwani sisi tunafaa wazi kwamba Ndoa ni mume na mke”, alisema Karama.
Wakati huo huo vuguvugu hilo liliahidi kuendelea kupinga dhulma za kingono na kutaka jamii kujitokeza na kuripoti visa hivyo ili kuwalinda watoto dhidi ya uovu huo.
Kauli hizo zilijiri baada ya Mahamakama kumuachilia jamaa mmoja anayedaiwa kumlawiti kijana wa miaka 12 kwa dhamana ya shilingi nusu milioni wakisema dhamana hiyo ni ndogo mno.
Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version