News

Wanaharakati wapinga nishati ya Nyuklia, Uyombo

Published

on

Mkurugenzi wa Shirika la Centre for Justice, Governance & Environmental Action, Phyllis Omido alisema nishati ya Nyuklia inayopania kuwekezwa katika eneo la Uyombo wadi ya Matsangoni kaunti ya Kilifi ni bei ghali mno.

Omido, alipinga vikali semi za serikali kwamba nishati hiyo itakuwa ya bei nafuu.

Akizungumza eneo la Matsangoni, Omido alikariri kwamba nishati hiyo itagharimu serikali fedha nyingi kufanikisha mradi huo kinyume na inavyodaiwa kwa sasa.

Omido alitolea mfano taifa la Afrika Kusini ambalo tayari limetekeleza uwekezaji wa Nyuklia hiyo, akisema kwamba bado linapitia masaibu mengi ya ukosefu wa nishati licha ya uwekezaji huo.

“Ripoti za utafiti wa kitaifa na kimataifa zilionyesha kuwa Kenya bado haina uwezo wa kufanya uwekezaji wa nishati ya Nyuklia.” aliongeza Omido.

Omido ambaye pia ni Mwanamazingira alisisitiza haja ya wakaazi kutokubali kulazimishiwa miradi ambayo ina athari kubwa kwa mazingira ya jamii.

Shughuli za uvuvi na ukulima zinatarajiwa kuathirika Zaidi iwapo mradi huo utafanyika katika eneo hilo la Uyombo na viungani vyake.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version