Sports
Wanaridha Beatrice Chebet,Faith kipyegon,Emmanuel Wanyonyi na Lilian Odira warejea kutoka Tokyo
Mabingwa wa Dunia Faith Kipyegon, Beatrice Chebet, Lillian Odira na Emmanuel Wanyonyi wamerejea nyumbani leo kutoka Tokyo, Japan, walikoshiriki mashindano ya Riadha Duniani.
Familia, ndugu, jamaa na rafiki pamoja na maafisa wa serikali walijitokeza kuwapokea mashujaa hao katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Wakizungumza, Kipyegon na Chebet walisema wanaazimia kusalia katika mbio za uwanjani kabla ya kuhamia barabarani.
“Nafurahia sana kushinda dhahabu ya nne katika mbi za mita 1,500 na pia kuwamotisha akina dada wengine kwa sababu mimi ni kama mama yao. Beatrice amekuwa akitazama nikikimbia, na saa hii tunakimbia naye,” akasema Kipyegon.
Aidha Chebet amesema aangazia kushinda medali zaidi katika mita 5,000 na 10,000, huku akisema ushirikiano wa kikosi cha Kenya ulichangia matokeo.
Odira amesema anajipanga sasa kushiriki mashindano ya Ultimate mwaka ujao baada ya kutwaa ubingwa wa Dunia.
Kenya ilimaliza ya pili katika msimamo wa nishani kwa dhahabu 7, fedha 2 na shaba 2.