News

Watu 6 wakamatwa kwa wizi wa mitihani ya KCSE

Published

on

Watu 6 zaidi wamekamatwa na maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI Kwa kuhusika na wizi wa mitihani ya kitaifa ya KCSE katika maeneo mbalimbali humu nchini.

Visa hivyo vya hivi punde vimeripotiwa katika kaunti za Pokot Magharibi, Bomet na Garissa huku idadi ya jumla ya wale waliokamatwa kwa wizi wa mitihani ya KCSE ikiwa ni watu 45.

Waliokamatwa kwenye kesi hizo za udanganyifu wa mitihani ni pamoja na wasimamizi wa mitihani, walimu na wanafunzi ambapo watu wanne wamekamatwa katika kituo cha mitihani cha Kapchemogen huko Pokot Magharibi.

Wengine ni pamoja na Wanafunzi wa shule ya upili ya Oreiyet iliyoko eneo la Chepalungu huku mshukiwa wengine aliyefahamika kwa jira la Eric Uoko akikamatwa katika kaunti ya Garissa baada ya kuwalaghai maafisa wa mitihani kwamba anafanyakazi katika baraza la mitihani nchini KNEC.

Wizara ya elimu nchini kupitia Waziri Julius Migos Ogamba imeonya kwamba itazidi kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na visa vya udanganyifu wa mitihani nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version