News
Wauguzi wagoma Kilifi
Mamia ya wauguzi kaunti ya Kilifi wamegoma na kufanya maandamano katikati mwa mji wa Kilifi.
Wauguzi hao wanalilia haki yao ikiwemo mishahara pamoja na kurejeshwa kazini kwa wauguzi wengine 21 waliosimanishwa kazi wakati wauguzi hao walipogoma kwa mara ya kwanza Julai 2025.
Miongoni mwa madai mengine ni kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba walioafikiana na Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Maitha Mung’aro mnamo Agosti 15 walipofutilia mbali mgomo wao pamoja na kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba wa makubaliano wa mwaka 2025.
Wauguzi hao wamaandamana hadi katika ofisi za Gavana wa Kilifi kuwasilisha nakala ya ombi lao huku akisema kwamba iwapo matakwa yao hayatimizwa basi itawalazimu kuendelea na mgomo wao.
Wakiongozwa na Katibu mkuu wa Muungano wa wauguzi tawi la Kilifi, wauguzi hao walilalamikia kuhangaishwa na utawala wa Gavana Mung’aro, kutotimizwa na maslahi yao pamoja na kuboreshwa kwa mazingira bora ya kazi.
Mgomo huo wa wauguzi tayari umesambaratisha kitengo cha akina mama kujifungua, kitengo cha huduma za dharura, kitengo cha mpango wa uzazi miongoni mwa huduma zengine.
Taarifa ya Eric Ponda