News

Wauguzi wanamtaka Gavana Timamy kutatua maslahi yao

Published

on

Muungano wa wauguzi katika kaunti ya Lamu ukiongozwa na Erick Otieno umekosoa kitendo cha maafisa wa polisi cha kuwatupia vitoa machozi walipoandamana kuelekea makao makuu ya kaunti ya Lamu eneo la Mokowe kuwasilisha malalamishi yao kwa gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdalla Timamy.

Otieno alisema kwamba ni mara ya tatu sasa tangu kuanza kwa mgomo huo wiki iliyopita na kila wanapotaka kuonana na gavana Timamy wanazuiliwa.

“Hii ni mara ya tatu tunazuiliwa na polisi ili tusimuone mwajiri wetu mkuu’’, alisema Otieno.

Kulingana na Otieno hali hiyo inaonyesha wazi kuwa serikali ya kaunti ya Lamu haiko tayari kushughulikia matakwa yao huku wakiapa kufika katika ofisi ya gavana Timamy mara kwa mara hadi watakaposikizwa.

Vilevile, Wauguzi hao walitoa wito kwa maafisa wa polisi kuzingatia sheria katika kutekeleza majukumu yao na sio kutumika visivyo katika kuwahangaisha wale ambao wanatafuta haki.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version