News
Wavuvi Kilifi waandamana kupinga Sheria za uvuvi
Wavuvi kutoka maeneo ya uvuvi ya mjini Kilifi waliamkia maandamano hadi nje ya lango la makazi ya Gavana Gideon Mung’aro kwa lengo la kumuona Gavana na kuwasilisha malalamiko yao.
Kilio cha ni kutaka kuondolewa kwa sheria za kupiga marufuku utumiaji wa mitego ya zamani ya kuvulia samaki baharuni.
Waandamanaji hao wakiwa na malengo ya kupata suluhu kuhusu malalamiko yao walifikia na taarifa kwamba Gavana Mung’aro alisafiri na malalamiko yao yakapokelewa na msaidizi wake
Aidha walisema kwamba tatizo lao ni uongozi kuhusu shughuli zao.
Hata hivyo hawakuridhika na majibu hayo na wakaendelea na maandamano yao hadi Old Ferry japo Gavana Mung’aro ilimtuma Msemaji wa serikali ya kaunti ya Kilifi Johnathan Mativo kupokea nakala walizokuwa pamoja na malalamiko yao.
Wakati huo huo Mbunge Kilifi Kazkazini Owen Baya alisema atashughulikia suala lao bungeni kupitia mswada unaokaribia kujadiliwa kuhusu sheria za uvuvi.
Taarifa ya Lolani Kalu