News

Waziri Oparanya aandamwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadam

Published

on

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu sasa wanataka kukamatwa kwa waziri wa vyama vya ushirika Wycliffe Oparanya kufuatia uamuzi wa mahakama kuu kuwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka alikiuka sheria kusitisha kesi dhidi yake.

Mashirika hayo yalimtaka mkurugenzi mkuu wa mashtaka kuwasilisha mashtaka mapya kulingana na uchunguzi wa tume ya kukabili ufisadi nchini EACC na uamuzi wa mahakama.

Aidha walimtaka kukomesha kile wanachodai mi kuingilia kati kazi za asasi na uchunguzi, vile vile kuheshimu majukumu ya EACC.

Katika uamuzi wake Jaji Benjamin Musyoki alitupilia mbali uamuzi wa mkurugenzi mkuu wa mshtaka akisema ulikiuka sheria.

Oparanya alitarajiwa kukabiliwa na mashtaka ya ufisadi wa shilingi miliongi 56.7 alipokuwa gavana.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version