Sports
Waziri Wa Michezo Salim Mvurya Asema Kenya Iko Tayari Kwa CHAN
SIKU 3 ZIMESALIA KUNGOA NANGA KOMBE LA CHAN:
Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya CHAN, Nicholas Musonye, wamefanya ukaguzi wa mwisho leo katika viwanja vya Kasarani na Nyayo kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Harambee Stars na DR Congo itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Kasarani.
Waziri Mvurya, akizungumza katika Uwanja wa Nyayo, amesema kuwa fursa hiyo ni ya kipekee kwa taifa na sekta ya michezo kwa ujumla, huku maandalizi ya kuelekea AFCON 2027 yakiendelea.
Aidha, Mvurya amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushangilia timu ya taifa, Harambee Stars, katika mechi ya Jumapili na michezo yote ya michuano hiyo.
Harambee Stars itacheza mechi zake zote katika Uwanja wa Kasarani. Timu hiyo imo katika Kundi A pamoja na Angola, Morocco, Zambia, na DR Congo.