Business
Wizi wa mavuno Shambani watajwa kukithiri
Mzee wa mtaa eneo la Mavueni kaunti ya Kilifi Catherine Anzazi amewaonya vijana wadogo dhidi ya kujiingiza kwenye makundi ya kihalifu.
Akizungumza na Coco Fm, Anzazi alisema kuwa vijana wengi wadogo ambao wengine wao ni wanafunzi wamekuwa na hulka ya kujiunga na makundi ya kihalifu hali anayoikemea vikali.
Anzazi alisema msimu huu wa mavuno kumekuwa na visa vya wakaazi wengi kuibiwa Mahindi hasa nyakati za usiku, matukio yanayotekelezwa na vijana hao.
Mzee huyo wa mtaa alihoji kwamba watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha hulka hiyo mbaya.
“Utumizi wa Mihadarati kama vile bangi ndio unaochochea baadhi ya vijana hawa kujiingiza kwenye uhalifu”, alisema Anzazi.
Aidha aliwashinikiza wakaazi wa eneo hilo pia kushirikiana na asasi za usalama katika kuwawajibisha wahalifu, akisema kuwa wengi wa wale wanaotekeleza wizi ni watu wanaojulikana.
Taarifa ya Hamis Kombe