International News

Al-Shabab yawaua wanajeshi 47 wa Uganda

Published

on

Kundi la wanamgambo la Al-Shabab kutoka nchini Somalia limesema liliwaua wanajeshi 47 wa Uganda wanaofanya kazi chini ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika wa Kusaidia na Kudumisha Utulivu nchini Somalia (Aussom) Jumatatu Agosti 4, 2025.

Taarifa zilisema shambulio hilo la bomu la kujitoa mhanga lilitekelezwa karibu na mji wa kilimo wa Barire.

Al-Shabab ilitoa taarifa ikidai kuwa pia walijeruhi wengine 31 na kuharibu magari tisa ya kijeshi.

Redio ya jeshi la Somalia ilisema kwamba vikosi vya Somalia na Aussom vilikamata na kuharibu magari mawili yaliyojaa mabomu kabla ya kushambulia kambi ya jeshi karibu na Barire.

Mji huo, ulioko kusini mwa Somalia katika eneo la Lower Shabelle, ulitekwa na al-Shabab wakati wa shambulio lililofanyika mwezi wa Ramadhani mnamo mwezi Machi 2025.

Tarehe 3 Agosti 2025, Aussom ilitangaza kwamba imeanzisha shambulizi kubwa la kuuchukua mji wa Barire na kukanusha ripoti za vyombo vya habari zinazodai kuwa idadi kubwa ya wanajeshi wake walijeruhiwa.

Mji huo uko umbali wa kilomita 50 kusini magharibi mwa Mogadishu na hutumika kama kituo cha mashambulizi ya wanamgambo, ikiwa ni pamoja na mji mkuu.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version