News

Askofu Mwero: Mizozo ya ardhi inafaa kukomeshwa Pwani

Published

on

Viongozi wa kidini katika ukanda wa Pwani wamejitokeza na kushinikiza kuchukuliwa kwa hatua za haraka kuhusu jinsi ya kukomesha changamoto zinazoathiri maisha ya wananchi mashinani.

Mwenyekiti wa Muungano wa Makanisa nchini NCCK tawi la Pwani Askofu Peter Mwero alisema migogoro ya ardhi, mihemko ya kisiasa, ukiukaji wa katiba, ukabila miongoni mwa masuala mengine yanafaa kukomeshwa.

Akizungumza katika kikao cha kutathmini masuala mbalimbali ya kaunti ya Kwale, Askofu Mwero alisema ongezeko la visa vya dhuluma za kijinsia katika jamii vinafaa pia kukomeshwa ili kuiwezesha jamii kuishi kwa amani.

“Haya ni mambo ambayo sio mazuri katika jamii yetu katika mambo ya maendeleo, itabidi viongozi wa dini zote kuingalia suala hili na pia tuweze kupinga vikali vitendo kama hivi vya ulawiti na ubakaji ili kaunti ya Kwale tuwe na amani na tuweze kuendelea pamoja”, alisema Askofu Mwero.

Wakati huo huo amesema kama Kanisa wataendeleza hamasa za amani kwa jamii mashinani ili kuwaepusha vijana na visa vya uchochezi na migogoro ya kisiasa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wasiojali maslahi ya wananchi.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version