Sports
Bandari Yampiga kalamu kocha wake Ken Odhiambo baada ya mechi 2 Tu
Kilabu ya Bandari ya Pwani imetangaza kumpiga kalamu kocha wake mkuu Ken Odhiambo baada ya mechi mbili pekee usukani msimu huu.
Haya yanajiri saa chache tu baada ya kilabu hiyo kupoteza goli 1-0 dhidi ya Shabana siku ya Jumapili ugani Mbaraki kaunti ya Mombasa.
Mwalimu huyo aliongoza The Dockers kumaliza nafasi ya nane msimu jana na alama 44 matokeo ambayo hayakupokelewa vema na uongozi wa kilabu hiyo.
Hata hivyo licha ya kupewa nafasi kubadilisha mambo baada ya kupata wachezaji wapya matokeo yanaonekana vinginevyo kilabu hiyo ikiwa na alama moja pekee kutokana na mechi 2 za FKF PL.
Naibu kocha John Baraza amepewa usukani wa kuongoza kilabu hiyo huku harakati ya kusaka kocha mpya kilabuni humo ikianza rasmi wadadisi wakisema kilabu hiyo sasa inasaka kocha wa kigeni.
Mechi ijayo ya kilabu hiyo ni dhidi ya Muranga Seal.