News
Bunge la kaunti ya Kilifi linarejelea vikao vyake Rasmi
Bunge la kaunti ya Kilifi linarejelea vikao vyake Agosti 4, 2025 baada ya kuahirishwa kwa mda wa majuma mawili.
Hii ni baada ya bunge hilo mnamo Julai 21, 2025 kuandaa kikao maalumu cha kupiga kura ya kujaza nafasi ya spika wa bunge hilo, iliyowachwa wazi baada ya wawakilishi wadi kumbandua mamlakani Teddy Mwambire Juni 30, 2025.
Katika uchaguzi huo Catherine Kenga aliibuka mshindi kwa kuapata kura 41 dhidi ya 51 na kuwashinda wapinzani wake wengine 4.
Mwishoni mwa wiki jana Kenga alitangazwa rasmi kupitia gazeti la serikali kama spika wa bunge la kaunti ya Kilifi na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhfa huo katika kaunti hiyo.
Majukumu ya kwanza kwa Spika huyo ni kuunganisha bunge hilo ambalo limeonekana kugawanyika kufuatia hoja iliyowasilishwa na kiongozi wa wachache Tom Chengo wa chama cha PAA ya kumuondoa mamlakani Mwambire.
Taarifa ya Joseph Jira