Sports

FIFA Yapiga Marufuku Bafana Bafana kwa Kumchezesha Mchezaji Asiyestahili 

Published

on

Shirikisho la FIFA imewapunguzia alama Bafana Bafana ya Afrika Kusini baada ya kisa cha kumchezesha Teboho Mokoena kinyume cha sheria kwenye mechi ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Lesotho miezi minne iliopita .

Timu hiyo ya taifa la Afrika Kusini pia imepigwa faini ya CHF 10,000 (takriban $10,800 USD), huku Mokoena akipewa onyo rasmi.

Kiungo huyo alipaswa kukosa mechi dhidi ya Lesotho kutokana na adhabu ya kadi za njano, lakini bado alichezwa.

 Adhabu hii ni pigo kubwa kwa ndoto za Bafana Bafana katika harakati za kufuzu Kombe la Dunia la FIFA.

Timu hiyo sasa ikishuka hadi nafasi ya pili kwenye jedwali la Kundi C na alama 14 Benin ikichupa kileleni kwa ubora wa magoli licha kuwa na alama 14 pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version