Sports
FIFA Yapiga Marufuku Bafana Bafana kwa Kumchezesha Mchezaji Asiyestahili
Shirikisho la FIFA imewapunguzia alama Bafana Bafana ya Afrika Kusini baada ya kisa cha kumchezesha Teboho Mokoena kinyume cha sheria kwenye mechi ya kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Lesotho miezi minne iliopita .
Timu hiyo ya taifa la Afrika Kusini pia imepigwa faini ya CHF 10,000 (takriban $10,800 USD), huku Mokoena akipewa onyo rasmi.
Kiungo huyo alipaswa kukosa mechi dhidi ya Lesotho kutokana na adhabu ya kadi za njano, lakini bado alichezwa.
Adhabu hii ni pigo kubwa kwa ndoto za Bafana Bafana katika harakati za kufuzu Kombe la Dunia la FIFA.
Timu hiyo sasa ikishuka hadi nafasi ya pili kwenye jedwali la Kundi C na alama 14 Benin ikichupa kileleni kwa ubora wa magoli licha kuwa na alama 14 pia.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

