Sports
Florian Wirtz Sasa Ni Mali Ya Liverpool
Ni Rasmi kwamba kilabu ya Liverpool imetangaza kupata sahihi ya kiungo wa taifa la Ujerumani na kilabu ya Bayern Leverkusen Florian Wirtz kwa dau la Euro milioni 150.
Mchezaji huyo anakua sajili wa pili kwa kocha Arne Slot na mchezaji ghali katika historia ya kilabu hiyo na miongoni mwa wachezaji 10 waliosajiliwa na donge nono zaidi barani ulaya nyuma ya Neymar na Mbappe ambao wote sajili zao zilikua za kihistoria.
Tineja huyo mwenye umri wa miaka 22 alishinda mataji matatu msimu wa mwaka 2023/24 chini ya kocha Xabi Alonso akifanikiwa kucheka na wavu mara 57 kutoka mechi 197 na kupiga pasi 65 kwa wenzake.
Wirtz anakua ndiye mchezaji ghali wa taifa la ujerumani na ligi ya Bundesliga akiwa pia ghali kusajiliwa ligi ya Epl.