News

Furaha Chengo:Sijaagizwa nijiondoe kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo Magarini

Published

on

Mgombea wadhifa wa ubunge katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi kupitia chama cha DCP Furaha Chengo Ngumbao almaarufu Kalama Wehu, amekana kupokea maagizo ya kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo eneo hilo la Magarini ulioratibiwa kufanyika mwezi Novemba 27, 2025.

Katika mahojiano kwenye kipindi cha Coco asubuhi, Kalama Wehu aliseme hajapokea maagizo yeyote ana iwapo hilo litatokea, ataendelea na harakati zake za kugombea wadhifa huo.

Matamshi ya Chengo yanajiri kufuatia madai kuwa mgombea huyo aliagizwa ajiondoe kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na kesi inayomkabili mahakamani.

Mwanaharakati huyo wa kisiasa alisema anaimani ya kuibuka na ushindi katika uchaguzi huo mdogo japo wapinzani wake wamekuwa wakitumia mbinu fiche za kuhujumu harakati zake za kuwania kiti hicho.

“Sijawahi kuitwa na mambo kama hayo na nikiitwa sinitakuwa nimeitwa? na uamuzi utakuwepo? wa kwamba mimi sishuki na nikishuka nitashuka na watu wa Magarini, yaani wanatafuta mbinu yeyote na walinitega kutoka kitambo, hii kushikwa na kufungwa vitu ambavyo havina hata kesi vimekuwepo kwa sababu wakiangalia watu mashinani wamewakataa”,alisema Chengo.

Wakati huo huo Chengo aliahidi kuboresha uchumi wa eneo hilo iwapo ataibuka na ushindi, kwa kuondoa ada za mashamba ili kuwapa nafasi wakaazi kujiendeleza kiuchumi kupitia kilimo.

“Kutoka mimi nizaliwe Magarini uchumi ulioko pale ni ule wa chumvi pekeyake ilihali tuko na nafasi ya kuwekeza viwanda vingi sana pale ndani ya Magarini, kuna sehemu zimefika umeme, zimefika barabara, zimefika maji, kumaanisha kwamba tukiweka viwanda vinaweza kufanya vizuri na wakaazi wapate ajira”,aliongeza mwanaharakati huyo.

Furaha Chengo alikamatwa kwa madai ya kuhusika katika maandamano ya kizazi cha Gen Z ya tarehe 25 mwezi Juni 2025, yaliyofanyika mjini Malindi na kusababisha vurugu zilizopelekea kuvunjwa kwa jengo la Al Noor, kunakopatikana makao makuu ya Ofisi za NSSF tawi la Malindi.

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kuwa na ushindani makali baada ya vyama vya kisiasa kuwakabidhi vyeti wagombea wao waliotangaza nia ya kuwania wadhfa wa ubunge wa Magarini.

Katika uchaguzi huo mdogo, bendera ya chama cha ODM itapeperusha Harrison Garama Kombe anayelenga kutetea kiti chake baada ya ushindi wake kubatilishwa na Mahakama kuu.

Harrison Kombe anayegombea wadhfa wa ubunge Magarini kupitia chama cha ODM.

Chama cha Wiper kilimpa cheti Samuel Nzai kuwania wadhfa huo, huku chama cha UDA kikiwakilishwa na Stanley Karisa Kenga.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version