News

Gachagua amshtuma IG Kanga kuhusu usalama wa Ol Kalou

Published

on

Kinara wa Chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, amemshutumu Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, kwa kusimamia operesheni ya usalama inayodaiwa kulenga kuvuruga uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Ol Kalou utakaofanyika siku ya Alhamisi, Julai 16, 2026

Gachagua alidai kwamba kupelekwa kwa zaidi ya maafisa wa polisi 1,000 kunalenga kushawishi matokeo ya uchaguzi huo kuegemea upade mmoja wa mrengo wa kisiasa.

Katika barua aliyomuandikia Inspekta Jenerali siku ya Jumatano Julai 15, 2026, Gachagua alidai kwamba uongozi wa huduma ya kitaifa ya Polisi umeingiliwa na kuathiriwa, na kwamba operesheni za usalama zinaelekezwa na maafisa wakuu serikalini badala ya uongozi wa maafisa wa Polisi.

Aidha alitilia shaka idadi ya maafisa wa polisi wanalitumwa eneo hilo, akisema ni sawa na kuhujumu haki za wakaazi wa Ol Kalou huku akisisitiza kwamba eneo bunge hilo limekuwa la amani kwa miaka mingi.

Kiongozi huyo alisema matukio yalioshuhudiwa katika eneo bunge hilo wakati wa kipindi cha kampeni za uchuguzi huo, yalilenga wafuasi wa Chama cha DCP.

“Inspekta Jenerali Kanja, inaonekana bado hujaelewa; uongozi wa Huduma ya kitaifa ya Polisi umechukuliwa kabisa na Kipchumba Murkomen, Raymond Omollo na wanasiasa waasi wanaomuunga mkono William Ruto,” alisema.

Gachagua ambaye alikuwa kuwa Naibu rais, alisema tabia ya maafisa wa polisi kukosa kuwachukulia hatua wahuni ni sawa na kuruhusu taifa kuingia katika utawala wa wahuni jinsi ilivyoshuhudiwa nchini Haiti.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version