News
Gavana wa Kericho Eric Mutai abanduliwa mamlakani
Gavana wa kaunti ya Kericho Eric Mutai amebanduliwa mamlakani kupitia hoja ya kutokuwa na Imani naye.
Jumla ya Wawakilishi wadi 33 kati ya 47 wa bunge la kaunti hiyo waliunga mkono hoja ya kumuondoa mamlakani.
Kikao hicho maalum kilizua mjadala mkali kabla ya kura kupigwa huku mivutano ya kisaisa ikishuhudiwa wakati wa kura hiyo na kupelekea Wawakilishi wadi wawili wa kaunti hiyo kujeruhiwa na kupelekea hospitalini.
Mutai anakabiliwa na shtuma za kutumizi mbaya wa mamlaka, kujinufaisha binafsi na miradi ya umma, ukiukaji wa Katiba na usimamizi mbaya wa rasilimali za kaunti hiyo.
Hatua hiyo imetokea siku ya mwisho ya kongamano la Ugatuzi la kutathminu ufanisi na changamoto za utawala hali ambayo inamuweka Gavana Mutai hatima yake kuwa mikononi mwa bunge la Seneti.

Vikao vya bunge la kaunti ya Kericho
Wakati wa kongamano hilo aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga kwenye hotuba yake aligusia migogoro ya uongozi baina ya magavana na Wawakilishi wadi hali inayoathiri Serikali za Ugatuzi, malengo na mchango mkubwa uliokusudiwa kuimarisha maendeleo Mashinani.
Taarifa ya Eric Ponda