News

“Handshake” ya Rais Ruto na Gedion Moi

Published

on

Rais William Ruto amevunja kimya chake na kuweka wazi kuhusu mkutano wa faraja uliandaliwa kati yake na Mwenyekiti wa chama cha KANU Gedion Moi katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne.

Rais Ruto alisema masuala walioafikiana ni pamoja na Gedion Moi kujiunga na serikali jumuishi yaani Broad-based Government, akitetea hatua ya Gedion kujiondoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa useneti, kaunti ya Baringo.

Akizungumza katika eneo la Kabarak kaunti ya Nakuru wakati wa mkutano na viongozi wa chama cha KANU, Rais Ruto alisema asilimia 90 ya wakenya wanamiliki nyumba, na kwamba ushirikiana wake na Gedion utasaidia kuafikia matakwa ya wakenya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha KANU, Gedion Moi alisema ushirikiano wa viongozi hao wawili unalenga kufanikisha malengo ya wananchi na kwamba hatua hiyo imemfanya kufanya maamuzi ya kujiondoa katika uchaguzi mdogo wa useneti wa Baringo.

Rais William Ruto na Mwenyekiti wa chama cha KANU katika mkutano wa wajumbe wa chama hicho eneo la Kabarak kaunti ya Nakuru

Hata hivyo wandani wa kisiasa wa viongozi hao wawili walisema ushirikiano wa Rais Ruto na Gedion Moi ni kuhakikisha familia ya Moi inapata ulinzi wa raslimali zao pamoja na masuala mengine ya ndani hasa maslahi ya kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version