News

Huenda hali ya ukosefu wa maji kaunti ya Kwale ikadhibitiwa

Published

on

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani amefungua rasmi upanuzi wa bomba la Moyeni-Kwa Lukongo eneo bunge la Kinango lenye urefu wa kilomita 2 ambalo litasaidia zaidi ya familia 260 ili kudhibiti hali ya ukosefu wa maji.

Achani amesema serikali ya kaunti ya Kwale inaweka mikakati zaidi kuwekeza kwenye sekta ya maji ili wenyeji wapate maji safi ya matumizi hasa kwenye baadhi ya maeneo kame kama ya Kinango, Lunga Lunga na Samburu.

Aidha, Achani amesema watahakikisha kaunti ya Kwale inaimarika zaidi katika masuala ya maendeleo kwa manufaa ya wenyeji.

Kwa upande wa wenyeji wa Moyeni wakiongozwa na Mwanasiti Mwahozi wameishukuru serikali ya kaunti ya Kwale kutokana na juhudi zake za kuhakikisha miradi ya majei inatekelezwa kwani kwa miaka mingi wamekuwa wakihangaika kutembea mwendo mrefu kusaka maji.

Kufikia sasa kaunti ya Kwale imechimba zaidi ya mabwawa 20 kwenye maeneo kame ya kaunti hiyo na zaidi ya visima 40.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version