News

IEBC inalenga vijana wa Gen Z katika zoezi la usajili wa wapiga kura

Published

on

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inatarajiwa kuanza rasmi zoezi la usajili wa wapiga kura wapya kote nchini, Septemba 29 mwaka huu huku ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Erastus Ethekon alisema zoezi linalenga kusajili vijana zaidi ya milioni 6.3, na litazinduliwa rasmi katika kaunti ya Kajiado siku ya Jumatatu.

Ethekon alisema zoezi hilo litatekelezwa pia katika vituo vya huduma Centre, na Ofisi za Tume ya IEBC katika maeneo bunge yote 290 kote nchini ili kuhakikisha idadi kubwa ya wakenya wanasajili hasa wale ambao bado hawajasajiliwa kama wapiga kura.

“Tunalenga kusajili idadi kubwa ya wapiga kura ambazo ni vijana wa Gen Z katika zoezi ambalo litaanza rasmi siku ya Jumatatu tarehe 29 mwezi Septemba, 2025 na tunawarai wakenya wote wale ambao hawajasajiliwa kutumia nafasi hii”, alisema Ethekon.

Wakati huo huo aliweka wazi kwamba Tume ya IEBC itahakikisha uchaguzi mkuu ujao unakuwa huru na haki, wakianda na chagunzi zote ndogo nchini zitakazofanyika Novemba 27 huku akiwarai wakenya kutopuuza zoezi hilo la usajili wa wapiga kura.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version