News

IEBC yasikitishwa na idadi ndogo ya wanaojisajili

Published

on

Tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, imeeleza kusikitishwa na idadi ndogo ya wananchi wanaojitokeza kujisajili kama wapiga kura tangu kuanza kwa zoezi hilo tarehe 29 Septemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa IEBC, Erastus Ethekon, alisema miongoni mwa changamoto zinazokwamisha usajili, ni umbali wa ofisi za tume hiyo na mchakato mrefu wa kupata vitambulisho vya kitaifa, na propaganda kwamba uchaguzi hautakuwa huru na wa haki.

Kufikia tarehe 31 mwezi Oktoba, IEBC ilisajili wapiga kura wapya 90,020 kote nchini, huku 15,619 wakihamisha kura zao, kaunti ya Mombasa ikisajili wapiga kura wapya 3,967 pekee, ikilinganishwa na lengo la wapiga kura wapya 183,000 .

Wakati huo huo Ethekon alishinikiza wakenya kupuuza madai ya wanasiasa kwamba wataiba kura zikiwemo za chaguzi ndogo.

Kwa upande wake, mkurugenzi mkuu wa tume ya IEBC, Hussein Marjan, aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujisajili na kutumia haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi wanaowataka.

Taarifa ya mwanahabari wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version