News
IEBC yawaidhinisha wagombea wa ubange wa Magarini
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC iliwaidhinishwa wagombea wa nafasi mbalimbali za changuzi ndogo zitakazoandaliwa Novemba 27 mwaka huu kabla ya kuanza rasmi kampeni
Katika kaunti ya Kilifi, wagombea zaidi ya 11 ambao wanamezea mate kiti cha ubunge wa Magarini waliwasilisha stakabadhi zao kwa Tume ya IEBC ili kuidhinishwa rasmi na kupewa cheti za kuwania wadhifa huo.
Stanley Karisa Kenga wa Chama cha DCP, Samuel Kombe Nzai wa chama cha Wiper, Furaha Ngumbao Chengo wa chama cha DNA ni kati ya viongozi walioidhinishwa na Tume ya IEBC katika ofisi cha Tume hiyo zilizoko mjini Malindi.
Wengine waliopata nafasi ya uidhinishwa siku ya Jumatano tarehe 9 mwezi Oktoba ni pamoja na Hamadi Karisa Chadi wa chama cha Roots Party, Emmanuel Kitsao Kalama wa chama cha TWAP, na John Sulubu Masha wa chama cha Kenya Social Congress.
Wagombea wengine alipangiwa zoezi hilo la kuidhinishwa siku ya Alhamis baada ya kuwasilisha stakabadhi zao na kupigwa msasa na maafisa wa IEBC ambao watasimamia uchaguzi huo mdogo wa Magarini.
Hata hivyo mgombea wa kiti hicho kupitia chama cha Federal Party of Kenya Jacob Themo Kwicha amekosa kuidhinishwa na maafisa wa IEBC baada ya cheti chake ya kugombea kiti hicho kutoka kwa chama kuonyesha kwamba anawania kiti cha uwakilishi wadi.

Cheti cha Jacob Themo Kwicha, cha chama cha Federal Party of Kenya kilichosababisha kukosa kuidhinishwa na IEBC
Tayari kampeni za uchaguzi huo mdogo wa Novemba 27, zinatarajiwa kuanza huku idara ya usalama kaunti ya Kilifi chini ya Kamishna Josphat Biwot ikiwaangaza wanasiasa hao kufanya kampeni za amani.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi