News

Itikadi za kidini na mafunzo ya kupotisha shuleni

Published

on

Itikadi za kidini na mafunzo ya kupotisha, sasa zimeanza kupenya katika mazingira ya shule licha ya uovu huo kuonekana katika maeneo ya nyumba za ibada na kuchangia wasiwasi mkubwa kwa jamii mashinani.

Zaidi ya shule 17 katika wadi ya Sokoke eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi, zilizua gumzo baada ya shule hizo kuonekana kuwashawishi wanafunzi kukumbatia mafunzo ya dhehebu la kihindi la Krishna HOI kwa msingi kwamba linapokea msaada wa chakula kutoka kwa shirika moja lenye misingi ya Kihindi.

Miongoni mwa masharti yanayotolewa na Shirika hili ni kwamba wanaofaidika na chakula hicho ni sharti wazingatie maombi haya kabla ya kula chakula, bila ya kujali misingi yao ya kidini na utamaduni.

Na kutokana na hali ngumu na umaskini unaokithiri eneo hili la Ganze, shule nyingi zimekumbatia mpango huu na shule zinazoridhia masharti haya pia hupokea mabango haya yenye maandishi kwa lugha ya kihindi yanayopasa kukaririwa na wanafunzi.

Kulingana na masharti haya mabango haya yanapasa kutundikwa jikoni ambako maombi haya ni sharti kwa kila mwanafunzi wanapopakiliwa chakula.

Kinachoshangaza zaidi ni kwamba hata mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kahingoni yenye zaidi ya wanafunzi 200 ambayo inakisiwa kwamba ni kati ya shule zilizokuwa zikipokea msaada huo na kukumbatia mafunzo ya dini hiyo kihindi ya Krishna HOI.

Shule ya msingi ya Kahingoni eneo la Sokoke kaunti ya Kilifi ni miongoni mwa shule zinazoendeleza Itikadi za kidini na mafunzo ya kupotisha

Japo Lengo na madhumuni ya muhisani huyu halijabainika,tayari wakaazi wengi wa eneo hili wameingiwa na hofu ya kuhusidha mpango huu na visa vya itikadi, hasa ikizingatiwa matukio ya Shakahola na Kwa Binzaro eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.

Hata hivyo katika kikao na Wanahabari kuhusu hali halisi ya itikadi hizi za kidini katika mazungira ya shule, Kamishna wa kaunti ya Kilifi Josphat Biwot amesema mpango huo wa usambazaji wa chakula cha msaada kwa shule hizo usimamishwa.

Kamishna Biwot amesema walimu katika shule hizo husika watachukuliwa hatua za kisheria kwani serikali haikubaliana na itikadi za kidini shuleni.

Taarifa ya Eric Ponda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version