News
Jaji wa Mahakama ya Rufaa Fred Ochieng’ Andago ameaga dunia
Idara ya Mahakama nchini pamoja na Wanasheria wanaomboleza kifo cha Jaji wa Mahakama ya Rufaa Fredrick Ochieng’ Andago aliyefariki dunia siku ya Jumatano, Septemba 17, 2025
Jaji mkuu nchini ambaye pia ni Rais wa Mahakama ya Upeo Martha Koome alimtaja Marehemu kama Jaji aliyejitolea kuitumia idara ya Mahakama kikamilifu kwa kuzingatia muongozo wa Katiba.
Naye Naibu Jaji mkuu Philomena Mwilu, amesema idara ya Mahakama imepoteza Mwanasheria aliyejitolea kutekeleza majukumu yake kwa kuhakikisha haki na sheria inalindwa.
Hata hivyo Msajali mkuu wa Idara ya Mahakama nchini Winfrida Mokaya ilisema idara ya Mahakama impoteza mtu muhimu sana kwenye masuala ya sheria, akisema Jaji Ochieng’ ataendelea kukumbwa na wengi kutokana na juhudi zake.
Jaji Ochieng’, ambaye hadi kufariki kwake, alikuwa akihudumu kama Jaji wa Mahakama ya Rufaa katika Mahakama ya Nakuru, na atakumbukwa kama afisa wa Mahakama aliyejitolea kuitumikia Mahakama kwa uadilifu na aliyechangia mageuzi mengi kwenye idara ya Mahakama
Mnamo 2003, kazi yake ilichukua mkondo wa kihistoria alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, kwani kwa miaka mingi, aliongoza vitengo na vituo muhimu, ikiwa ni pamoja na kitengo cha biashara na ushuru jijini Nairobi, pamoja na vituo vya Mahakama Kuu katika maeneo ya Kitale, Kakamega, na Kisumu.
Jaji Ochieng’ pia aliwahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Kisumu kabla ya kupandishwa cheo hadi katika Mahakama ya Rufaa.
Mpango ya maandalizi ya mazishi imeanza huku tarehe rasmi ya mazishi ikitarajiwa kutangazwa baadaye na familia yake
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi