Sports
Jose Mourinho ‘akubali mkataba wa miaka miwili’ kujiunga na Benfica kama kocha mkuu
Mkufunzi mreno Jose Mourinho ameripotiwa kukubali kandarasi ya miaka miwili kuwa kocha mkuu wa Benfica, miaka 25 tangu alipohudumu kwa mara ya kwanza katika klabu hiyo.
Mourinho, mwenye umri wa miaka 62, amekuwa huru tangu alipofutwa kazi na Fenerbahce mwezi uliopita baada ya kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Upatikanaji wa Mreno huyo uliibua uvumi mkubwa kuhusu hatima yake, lakini ripoti mapema wiki hii zilimhusisha kwa karibu na Benfica baada ya klabu hiyo kumtimua aliyekuwa kocha wa Wolves, Bruno Lage.
Hali hiyo imeharakishwa ndani ya saa 24 zilizopita, na Mourinho alionekana akiwasili nchini Ureno Jumatano usiku akitokea Barcelona, akiweka wazi hatua ya kuelekea klabuni hapo. Na, kwa mujibu wa Sky Sports, Mourinho sasa amekubali kurejea katika timu iliyompa kazi yake ya kwanza ya ukocha mwaka 2000 – ambapo atasaini mkataba wa miaka miwili.
Mwaka 2000, Mourinho alisimamia mechi 10 pekee, lakini mabadiliko ya uongozi wa juu wa klabu yalisababisha yeye kuwasilisha barua ya kujiuzulu – kabla ya kuchukua nafasi ya muda wote katika klabu ya Uniao de Leiria.