News

Kenyatta awarai wanachama wa Jubilee kuwa na fikra pana

Published

on

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amewarai wafuasi na wanachama wa Chama cha Jubilee kuwa na fikra pana katika kuwachagua viongozi walio na maono ya maendeleo ili kufanikisha ajenda ya wananchi.

Kenyatta alisema kila mmoja na haki ya kupigania nafasi ya urais, bila kujali kabila, mrengo ama maeneo bali kwa kujali misingi ya ajenda ya maendeleo ya taifa, akisema kiongozi bora ni yule asiyepora na kutenga wengine.

Akizungumza katika mkutano wa chama hicho Ijumaa tarehe 26 mwezi wa Septemba 2025 baadfa ya kuufungua rasmi  jijini Nairobi, Kenyatta alisema atahakikisha tiketi ya chama inatolewa kwa haki na uwazi kwa wagombea wa nyadhfa mbalimbali ili kuhakikisha chama hicho kinapata viongozi bora.

Kenyatta aliahidi kushirikiana ipasavyo na wanachama wa chama hicho kuhakikisha kinazidi kuwa imara huku Jubilee ikipendekeza Fred Matiang’I kupeperusha bendera ya jubilee kuwania wadhifa wa urais 2027.

“Kuanzia sasa nitakuwa nanyi tukizuru mashinani kwa lengo la kuimarisha chama chetu na nawasisi tudumishe umoja kama alivyosema Kioni’’, alisema Uhuru Kenyatta.

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, Katibu mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni, aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiangi na viongozi wengine wakati wa mkutano wa chama cha Jubilee, Nairobi.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Jubilee nchini Jeremiah Kioni aliwahimiza wanachama wa chama cha Jubilee kuwa na umoja kwa ajili ya kipute cha uchaguzi mkuu ujao wa 2027.

Kioni alisema kuna baadhi ya changamoto ambazo ziliikumba chama hicho wakati na baada ya kuandaliwa kwa uchaguzi wa mwaka uliopita na ni lazima mikakati ifaayo iwekwe ili kushinda nyadhifa nyingi za uongozi 2027.

Kioni alisema kuna baadhi ya wanachama wa chama cha Jubilee ambao walichangia kwa chama hicho kuwa na migawanyiko na katiba ya chama itafanyiwa marekebisho ili kuhakikisha Jubilee iko thabiti.

“Ni lazima turekebishe katiba ya chama kama njia mojawapo ya maandalizi ya uchaguzi huo, maana kuna baadhi ya watu ambao hawakuwa wanaheshimu uongozi wa chama na walisababisha migawanyiko chamani’’ alisema Kioni.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version