Sports

Kilabu MTG United Imezindua Wachezaji 8 Wapya kabila ya msimu wa NSL

Published

on

Kilabu ya MTG United ya akina dada ya kaunti ya Kilifi inayoshiriki Ligi ya daraja la Pili NSL imewatambulisha wachezaji wanane wapya kuelekea msimu mpya. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo kinara ambaye pia ni naibu Gavana wa Kaunti ya Kilifi Flora Mbetsa Chibule amehakikishia Timu hiyo kwamba atatembea nao katika mechi Zote za Ligi msimu wa mwaka 2025/26.

“Nitahahakisha ninatembea nanyi katika kila mechi msimu huu,kuanzia na ya kwanza kule Kwale Oktoba 5 ,mimi na wenzangu tutakuja kuwasapoti kilabu yetu kufanya vizuri,kila ushindi mtakayopata nitaongeza posho.”

Mkurugenzi mkuu katika wizara ya michezo Boniface Kirimi amesema kwamba wizara pamoja na kaunti ziko tayari kuinua vipaji akisema kwamba serikali hiyo imo mbioni kuboresha miondo msingi.

“Kwa sasa serikali ya kaunti iko katika hatua ya mwisho mwisho kuendeleza ujenzi wa Uga wa Waters ,tunaunda pia viwanja viwili vya mchezo wa mpira wa vikapu na juzi tumekutana na shirikisho la FKF Kaunti ya Kilifi kuiweka mikakati ya kuboresha miondo misingi ya soka na kuwashika mkono vilabu vyetu.”

Afisa mkuu mtendaji wa MTG United Dorcas Amakobe amesema kwamba msimu huu wameweka mikakati kuhakikisha kwamba kilabu hiyo inapata ufanisi uwanjani akiahidi kwamba akina dada hao kando na kulipwa mshahara watapata marupurupu katika kila mechi wanayoshiriki.
“Ili timu yetu iweze kushiriki kikamilifu na kupata matokeo chanya kama shirika tumeamua kutenga kilabu ya MTG kupata maslahi ya kipekee kama idara,natoa ahadi pia kwamba kando na mishahara hawa wanadada watapata marupurupu ili kuwapa hamasa katika mechi zao.”
Kwa upande wake Kocha wa MTG United Fatima Khamis marufu coach Tibu ameahidi kupaisha Kilabu hiyo Hadi kileleni wakisaka tiketi ya ligi kuu Akina dada FKF WPL.
“Nina matumaini msimu ujao tunamaliza ya kwanza ama ya pili,lakini pia nimshukuru naibu gavana Chibule kwa kusapoti timu kwa hali na mali msimu jana,tumeweza kusajili wachezaji wanane wapya kwa ajili ya msimu mpya na tuna matumaini watatupa matokeo chanya.”
MTG United walimaliza nafasi ya Saba msimu wa mwaka 2025/26

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version