Sports

Kocha Fadlu aondoka Simba SC, ajiunga na Raja Casablanca ya Morocco

Published

on

Miamba wa soka wa Tanzania, klabu ya Simba, wameafikiana kuachana na kocha mkuu Fadlu Davids baada ya kuhudumu kwa mmoja pekee.

Kulingana na taarifa kwa umma, usimamizi wa Simba umetaja hatua hiyo kuwa ya maafikiano kati ya timu na Fadlu baada ya raia huyo wa Afrika Kusini kutaka aruhusiwe kuondoka.

Fadlu anaaminika kuomba kusitisha mkataba na Simba baada ya kusajiliwa na  miamba  Raja Casablanca ya Morocco.

Akiwa Simba Fadlu ambaye ni raia wa Afrika Kusini aliwaongoza Simba  kumaliza katika nafasi ya pili ligini na kucheza hadi fainali ya kombe la Shirikisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version