Sports

Mahakama Kuu ya Kakamega yatupilia mbali ombi la Patrick Matasi, FKF yapewa ruhusa kuendelea na nidhamu dhidi yake

Published

on

Mahakama Kuu mjini Kakamega imetupilia mbali ombi lililowasilishwa na mlinda lango wa zamani wa Harambee Stars, Patrick Matasi, hatua ambayo imeiruhusu rasmi Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kuendelea na hatua za kinidhamu dhidi yake kuhusiana na madai ya upangaji wa matokeo ya mechi (match-fixing).

Uamuzi huo ni ushindi mkubwa kwa FKF katika vita vyake dhidi ya udanganyifu kwenye soka, baada ya mahakama kuthibitisha kuwa shirikisho hilo lilitenda ndani ya mamlaka yake chini ya Kanuni za FKF za Kupambana na Upangaji wa Mechi.

Matasi alikuwa amewasilisha kesi mwezi Aprili 2025, na kupata amri za muda (conservatory orders) zilizozuia kwa muda FKF kutekeleza adhabu yake ya kusimamishwa kwa siku 90.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version