Sports
Matayarisho yamekamilika kwa Fainali ya Kusisimua ya Misruru ya Raga ya Wachezaji Saba kila Upande Jijini Kisumu
Shughuli zote ziko tayari kwa ajili ya fainali ya kusisimua ya Raga ya Taifa ya Mizunguko ya Saba mwaka 2025, itakayofanyika jijini Kisumu marufu kama Dala Sevens katika Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Mamboleo, kuanzia Septemba 13–14.
Kwa sasa, KCB RFC na Strathmore Leos wako kwenye pambano kali la kuwania ubingwa wa jumla, na macho yote yataelekezwa Kisumu ambapo mzunguko huu wa mwisho unatarajiwa kutoa burudani kubwa la raga na shangwe za mashabiki.
“Dala Sevens imekua na kuwa moja ya mashindano yenye ushindani mkubwa na yenye hisia nyingi nchini, na mwaka huu hautakuwa tofauti. Tupo tayari kukaribisha familia ya raga Kisumu kwa wikendi kubwa,” alisema Mwenyekiti wa Kisumu RFC, Gabriel Ouma, wakati jiji la kando ya Ziwa likijiandaa kwa fainali hiyo kubwa.
Akizungumzia maandalizi, Ouma alionyesha kujiamini katika kutoa uzoefu wa kipekee ndani na nje ya uwanja.
“Dala Sevens imekua kuwa moja wa mashindano makali na yenye mvuto mkubwa, na mwaka huu pia itakuwa hivyo. Tupo tayari kuwapokea mashabiki wa raga Kisumu kwa wikendi ya kukumbukwa.
“Ufadhili wa Tusker umechangia sana kuinua ubora wa mashindano haya, na tunatarajia mashabiki kujitokeza kwa wingi kufurahia raga ya kiwango cha juu na mazingira ya kipekee ya Dala Sevens.”
Mashindano ya mwaka huu yamepata msukumo baada ya Tusker kuthibitisha ufadhili wa Ksh milioni 3 kwa ajili ya kuunga mkono Dala Sevens.
Ushirikiano huu unaendeleza dhamira ya muda mrefu ya Tusker katika kudhamini raga ya Kenya na kusherehekea shauku na uvumilivu wa wanariadha wa nyumbani.
“Raga ina nafasi ya kipekee katika mioyo ya Wakenya, na Dala Sevens kila mara imekuwa tukio kubwa la msimu,” alisema Keza Mpyisi, Meneja wa Michezo wa Tusker Brand.
“Tunajivunia kusimama na Kisumu RFC na familia pana ya raga tunapokaribia tamati ya mzunguko huu. Kwa Tusker, si suala la kudhamini tu, bali ni kuwaleta mashabiki pamoja kusherehekea ubora, kipaji na roho ya michezo ya Kenya.”
Kwa sasa, KCB Rugby wanaongoza mzunguko kwa alama 104 na wanahitaji tu kufika nusu fainali ili kutwaa ubingwa, huku Strathmore Leos wenye alama 95 wakihitaji safari kamili ya ushindi Kisumu ili kuendeleza matumaini yao.
Makundi ya Dala Sevens:
-
Kundi A: Kabras Sugar, CUEA Monks, MMUST, Nakuru RFC
-
Kundi B: Daystar Falcons, MSC Rugby, Kenya Harlequin, Nondescripts
-
Kundi C: KCB Rugby, Mwamba RFC, Homeboyz RFC, Embu RFC
-
Kundi D: Strathmore Leos, Menengai Oilers, Impala RFC, Kisumu RFC