News

Mchungaji akamatwa kwa kuwalazimisha watoto kufunga kula katika kijiji cha Dera,Kilifi

Published

on

Idara ya usalama katika kaunti ya Kilifi imeanzisha uchunguzi baada ya kumkamata Mhubiri tata Kamanza Mwatela Kwa tuhma za mahubiri potovu ya kidini katika kijiji cha Dera eneo bunge la Kilifi Kaskazini.

Katika opareseheni hiyo, polisi walifanikiwa kuwaokoa watoto watano walikuwa wamedhohifika baada ya kulazimishwa kufunga kula na kunywa.

Afisa mkuu wa idara ya DCI kaunti ya Kilifi Robert Kiinge alisema Mhubiri huyo wa kanisa la Jesus Ministry alikuwa akiendesha ibada katika nyumba aliyokodi katika kijiji hicho baada ya kuhama kutoka mjini Malindi.

“Tunaendelea na uchunguzi kubaini kiini hasa cha Mchungaji huyo maana huwezi lazimisha watoto kufunga kula na kunywa”, alisema Kiinge.

Kwan upande wake Afisa wa watoto eneo la Kilifi Kazkazini Warren Apopo alisema baada ya kuwahoji watoto hao walibaini kwamba watoto walikuwa wakienda shule kama kawaida na hawakuwa wakifunga kula.

Apopo alifafanua kwamba huenda kuna tatizo la kifamilia katika hilo boma kwani Mchungaji huyo alikuwa amekaribishwa na mama mmoja aliyemuombea hadi akapona.

“Tuliwahoji watoto na kukagundua kwamba walikuwa wanaenda shule na pia hawakuwa wanafunga lakini kuna tatizo hapo kwa boma tunashuku tu mchungaji alikuwa na mahusiano na mama mmoja ndio kuna hizi tuhma”, alisema Apopo.

Wakaazi eneo hilo walisema walikuwa wakitilia shaka mafunzo ya mchungaji huyo kwa kuwazuilia watoto na kuwashawishi wazazi na watoto kupuuza masomo.

Kulingana na mzee wa kijiji hicho Alphonce Kahindi, mchungaji huyo aliwasili katika kijiji cha Dera mwezi wa pili mwaka wa 2025, na kuanzisha ibada zake katika nyumba aliyokodi kabla ya kuanza kuwashawishi watoto hao kufunga kula na kunywa.

Kahindi alidokeza kuwa hali hiyo ilimlazimu kuripoti kwa idara ya usalama ambao walifika na kuwaokoa watoto hao huku wawili kati yao wakiwa wamedhoofika zaidi kiafya baada ya kufunga kwa siku 6.

“Kuna mchungaji ambaye amefungia watoto ndani ya nyumba kwa ajili ya kuomba, sasa watoto wako humo na jana ilikuwa ni siku ya sita, hawajakula hawajakunywa, ikabidi nimpigie simu chifu wa Sokoni na nikapigia madam D.O, ikabidi madam D.O atume tayari gari yake na askari, tukakuja jana jioni na tukampata huyo mchungaji”, alisema Kahindi.

Tukio hilo linajiri wakati ambapo washukiwa kadhaa wanaendelea kuzuiliwa na polisi kuhusiana na madai ya mauaji ya watu katika eneo la Kwa Binzaro eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi kufuatia ushawishi wa dini potofu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version