Sports
Michael Olunga Aondoka Al-Duhail
Sasa ni rasmi kwamba mshambulizi wa timu ya soka Harambee Stars Engineer Michael Ogada Olunga ametangaza kuachana na waajiri wake kilabu ya Al- Duhail ya Qatar
Mwamba huyo alijiunga na kilabu hiyo msimu wa mwaka 2021 akitokea Keyshiwa Reysol ya japana na mpaka sasa amefanikiwa kuibuka mfungaji bora kwenye kilabu hiyo akifunga magoli 130.
Kupitia kwenye tuvuti ya kilabu hiyo Al-Duhail imeweza kumshukuru nyota huyo ambaye amefunga magoli 12 msimu huu na kuchangia mengine mawili katika mechi 19 ambazo amechezea kilabu hiyo
Nyota huyo amewahi shinda kiatu cha dhahabu akiwa mfungaji bora mwaka 2021-22 na magoli 22.
Vilabu vingine ambazo amechezea ni pamoja na Girona ya Uhispania,Djugardens ya Sweeden,Zhicheng ya Uchina na Keyshiwa Reysol ya Japan.
Mpaka sasa haijawekwa wazi kilabu yake mpya.