Sports

Mshambulizi wa PSG Ousmane Dembele ndiye Mchezaji bora tuzo ya Ballon d’Or ya wanaume katika sherehe iliyofanyika jijini Paris Jumatatu

Published

on

Mshambuliaji wa Ufaransa, Ousmane Dembele, ameshinda tuzo ya Ballon d’Or ya wanaume katika sherehe iliyofanyika jijini Paris Jumatatu, tuzo kubwa zaidi ya heshima binafsi katika soka, akitunukiwa kwa mchango wake mkubwa katika kikosi cha Paris Saint-Germain kilichotwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Dembele, mwenye umri wa miaka 28, amemshinda nyota chipukizi wa Barcelona na Uhispania, Lamine Yamal, katika kinyang’anyiro hicho na kumrithi kiungo wa Manchester City na Uhispania, Rodri, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2024.

Dembele, akiwa na hisia kali, alishindwa kuzuia machozi mara tatu wakati wa hotuba yake kabla ya mama yake kujiunga naye jukwaani.

  • Mshambulizi wa Arsenal, Viktor Gyokeres, alishinda tuzo ya Mshambuliaji Bora kutokana na ubora wake akiwa Sporting Lisbon ya Ureno msimu uliopita.

  • Gianluigi Donnarumma alitwaa tuzo ya Kipa Bora,

  • huku Kocha wa PSG, Luis Enrique, akitunukiwa tuzo ya Kocha Bora.

Dembele, aliyewahi kuchezea Borussia Dortmund na Barcelona, na aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwaka 2018, alifunga mabao 35 katika mashindano yote. PSG walitwaa Ligi ya Ufaransa, Kombe la Ufaransa, na kwa mara ya kwanza katika historia yao, Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Sina maneno ya kueleza… ulikuwa msimu wa kipekee na PSG,” alisema Dembele kwa hisia, akimuelezea kocha wake Luis Enrique kama “kama baba.”

“Hii ni tuzo ya mchezaji mmoja, lakini ukweli ni kwamba ilikuwa juhudi ya pamoja,” aliongeza Dembele, mmoja kati ya wachezaji tisa wa PSG walioteuliwa kwa tuzo hiyo.

“Ballon d’Or haikuwa lengo kubwa katika maisha yangu ya soka, lakini nilifanya kazi kwa bidii ili timu ishinde Ligi ya Mabingwa.”

Kwa upande mwingine, Lamine Yamal mwenye umri wa miaka 18, ambaye alikuwa mchezaji mwenza wa Dembele Barcelona alipoibuka mwaka 2023, alishinda tena Kopa Trophy kwa mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 21 — ikiwa ni mara ya pili mfululizo kutwaa heshima hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version