News

Mswada wa marekebisho ya Katiba wa mwaka 2026 umewasilishwa bungeni

Published

on

Mswada wa marekebisho ya Katiba wa mwaka 2026 na sheria za uchaguzi umewasilishwa katika bunge la Seneti.

Mswada huo unalenga kufanyia marekebisho kipengele cha Katiba cha 99 na 193 pamoja na sheria za uchaguzi sehemu ya 24 na 25 ili kuwepo na uwazi kwa magavana wanaolenga kuwania nyadhfa za uongozi baada ya kukamilisha mihula yao.

Mswada huo uliowasilishwa na Seneta wa Kirinyaga James Murango unalenga pia kuzuia magavana waliomaliza mihula yao ya uongozi kutowania nyadhfa za useneta, ubunge ama uwakilishi wadi, kwani inakuwa vingumu kuchunguzwa.

Kuwasilishwa kwa mswada huo bungeni kufuatia hali magavana kuwania wadhfa wa useneta baada ya kukamilisha mihula yao ya uongozi hali ambayo imeleta sintofahamu ya kiuongozi, ikiashiria tamaa za uongozi na njama ya kuhitilafiana na ufuatiliaji wa matumizi ya raslimali za umma.

Seneta Murango alisema katika utekelezaji wa majukumu yao, magavana hulazimika kuwajibika mbele ya mabunge ya kaunti na Seneti kuhusu matumizi ya kifedha na kiutawala.

Wakati huo huo alidokeza kwamba iwapo mswada huo utapishwa na kuwa sheria utasaidia kufutilia usimamizi wa raslimali za kaunti na matumizi ya fedha kwani utazuia magavana kuhitilafiana na uchunguzi.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version