Business
Mvua Yaua Soko la Mitumba Mariakani, Wateja Wapungua
Wafanyabiashara wa kuuza mitumba katika soko la Mariakani kaunti ya Kilifi wamelalamikia kupungua kwa biashara hiyo hasa musimu huu wa Mvua.
Akiongea na mwahabari wetu, Mwenyekiti wa soko hilo Mwasingo Ngura amesema kwamba wateja wengi kwa sasa wameingia kilimo hali inayopelekea ukosefu wa wateja kwenye soko hilo.
Kiongozi huyo wa Soko hata hivyo amesema kwamba wanaamini biashara hiyo itaboreka baada ya msimu huu wa mvua kumalizika.
Wakati huo huo Ngura ameendelea kuilaumu serikali ya kaunti ya Kilifi kwa madai ya kukosa kutambua wafanyabiashara wa soko hilo katika kuboresha soko hilo.