News

Naibu rais Prof. Kithure Kindiki amkosoa Uhuru Kenyatta

Published

on

Naibu wa rais Prof. Kithure Kindiki amemkosoa Rais mstaafu Uhuru Kenyata kutokana na matamshi yake dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza.

Akirejelea suala aliloibua rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuhusu mpango wa Linda Mama, Kindiki alisema mpango huo uliotekelezwa chini ya serikali ya Jubilee haukua wa kujumuisha wakenya wote.

Kindiki aliongeza kuwa bima mpya ya SHA inawafaidi wakenya wote bila ubaguzi.

Wakati huo huo Kindiki alimtaka rais huyo mstaafu kuikosoa serikali ya sasa kwa hekima badala ya lawama.

“Kuna watu wengi wanaleta mzaha kwa haya maneno ya afya ya umma, na wanaongea kiholela, na hawataki kusema hapo mbeleni hatukuwa na msingi dhabiti wa afya, sisi tunashukuru yale mambo rais William Ruto wakati alipokuwa naibu rais walianzisha na rais Uhuru Kenyatta mradi wa Linda Mama, sasa huu mradi mpya haumaanishi ya kwamba hatuka katika ule mpango wa kusaidi akina mama wajawazito kupitia Linda Mama”,alisema Kindiki.

Wakati huo huo viongozi wa kaunti ya Mombasa wakiongozwa na gavana Abdhulswamad Sharrif Nassir na mbunge wa Likoni Mishi Mboko, walishutumu viongozi wa upinzani wanaopinga miradi ya serikali, wakisema upinzani haujawakuwa na manufaa kwa mwananchi wa kawaida.

Viongozi hao walimkosoa moja kwa moja rais mstaafu Uhuru Kenyatta, wakidai kuwa anachochea siasa badala ya kutoa ushauri mwafaka kwa serikali iliyoko mamlakani.

Taarifa ya Elizabeth Mwende

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version