Sports

Novak Djokovic Kusaka Taji La 25 La Wimbledone Hii Leo

Published

on

Nyota wa mchezo wa Tenesi Ulimwenguni Novak Djokovic raia wa Serbia anaingia leo ulingoni kusaka taji la 25 la Wimbledon.

Hata hivyo mchezaji huyo anatarajiwa upinzani mkubwa kutoka kwa Carlos Alcaraz raia wa Uhispania ambaye anaorodheshwa wa pili kote ulimwenguni na Jennik Sinner anayeorodheshwa wa kwanza kote ulimwenguni.

Bingwa huyo ambaye ana mataji 24 kwa sasa akiwa kwenye kiwango kimoja na Magret Court anamini kwamba anauza kuwa Mwanatenesi wa kwanza kushinda taji la 25 na kuingia kwenye daftari za kumbukumbu kabla ya kustaafu.

Mshindi huyo mara nane wa tuzo hilo la Wimbledon amepoteza fainali mbili mfululizo kwa nyota wa Uhispania Carlos Alcaraz.

Djokovic anatarajiwa kufungua kampeini yake dhidi ya Alexandre Muller raia wa Ufaransa Leo Usiku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version