News

Rais Ruto aelekea Marekani kwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa

Published

on

Rais William Ruto ameondoka nchini Jumamosi 20, Septemba 2025, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 80 wa Umoja wa Mataifa mjini New York, nchini Marekani.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed alisema ajenda ya rais Ruto mjini New York itakuwa juu ya ushirikiano wa pande nyingi, kutetea mageuzi ya mfumo wa fedha duniani, na kutoa wito wa upatikanaji wa haki wa fedha za maendeleo kwa nchi zinazoendelea.

Pia rais atashinikiza mageuzi ya umoja wa Mataifa ili kujumuisha zaidi na kushughulikia changamoto za amani na usalama duniani, ikiwa ni pamoja na kuimarisha juhudi za amani katika matifa ya Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Somalia na Haiti.

Katika baraza kuu, kiongozi wa taifa pia anatarajiwa kutetea uwakilishi wa Afrika katika baraza la usalama la umoja wa mataifa, ambapo bara hilo lina uanachama usio wa kudumu pekee.

Chini ya majadiliano ya kiserikali juu ya mageuzi ya baraza la usalama la umoja wa mataifa, nchi wanachama zinapigania ongezeko la viti vya kudumu na visivyo vya kudumu, ili kuwa uwakilishi wa kweli wa chombo hicho cha kimataifa.

Katika wiki hiyo ya ngazi ya juu, Kenya pia inatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu misheni ya msaada wa usalama wa kimataifa ya Haiti, miaka miwili baada ya kutumwa kwa wanajeshi wake kuongoza misheni hiyo.

Taarifa Ya Joseph Jira

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version